Ijumaa, 5 Mei 2017

Bwanaharusi mbaroni


BWANA HARUSI ATIWA MBARONI KWA KUJAZA NDUGU FEKI UKUMBINI

====================================
BWANA harusi mchina, amekamatwa na polisi na sasa yuko rumande, baada ya kuhadaa wakwe zake kuwa amealika wageni 200, kumbe ni uongo watu hao wote ni wasanii wa kulipwa ukumbini.

Alipatwa na msukosuko huo baada ya familia ya mkewe kugundua kuwa watu aliokuwa anadai ni marafiki na ndugu zake, aliwapa ‘mshiko’ ili kuhudhuria harusi.

Kwa mujibu wa gazeti moja la jimbo la Kaskazini, nchini China, Polisi walimkamata Liu Wang., wakati ulipotokea mjadala kwenye mgogoro uliozuka baina yake na wageni ambao ilibainika ni marafiki tu, ingawa haikuwekwa wazi uhusiano wake nao.

Sherehe zilipoanza, hakukuwepo dalili za wazazi wa Liu kuwepo na ndipo joto la msuguano likaanza kupanda.

Mmoja wa wageni hao waalikwa wanaolipwa, aliiambia televisheni moja ya Shaanxi kwenye kipindi kiitwacho ‘guests’ kwamba walilipwa Yuan 80 ambazo ni sawa na Dola za Marekani 12 au sawa na Shilingi 25,000 au Pauni tisa, ambayo ni sawa na Shilingi 28,000 kutoka kwa bwana harusi - Wang.

Walisema walilipwa kwa kila siku waliyotumika ili wajifanye kama wanandugu zake .

Pia inadaiwa kuwa watu hao ni pamoja na madereva wa teksi, wanafunzi na maswahiba wengine wa bwana harusi huyo, kupitia mtandao wa kijamii wa jukwaa la ‘WeChat walijadiliana naye gharama za malipo kwa ushiriki wao kwenye harusi.

Bibi harusi alisema kuwa, amemfahamu mumewe huyo kwa zaidi ya miaka mitatu, ingawa hakufahamu chochote kuhusu utapeli wake.
Bado haijafahamika kile Liu anachokificha, licha ya kwamba hakuvunja sheria za nchi.

Baadhi ya vyombo vya habari vilidai kuwa, muoaji huyo alikuwa anatoka katika jamii maskini na katika kuficha uhalisia wake, aliamua kutosema ukweli kwa jamaa zake walioko vijijini, wasifike kwenye harusi, akihisi angeaibika.

Televisheni ya Kanda inayomilikiwa na serikali Xibu Online, imesema kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi.

Ijumaa, 21 Aprili 2017

TAKUKURU YAOKOA MIL 74/- SEMINA HEWA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Arusha imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh milioni 74.8 zilizolipwa kwa watumishi na semina hewa. Aidha watumishi wa umma wamesisitizwa kufanya kazi kwa maslahi ya umma, kwa kuzingatia suala zima la uadilifu na kuacha kuwashawishi wananchi kutoa fedha ili wapate huduma.
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Arusha, Frida Wikessy wakati alipotoa taarifa ya utendaji kazi wa tasisi hiyo katika kipindi cha Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu.
Wikessy alisema fedha hizo zimerejeshwa serikalini baada ya kuziokoa kutokana na watumishi hewa pamoja na semina hewa zilizoandikwa kwa kughushi saini ili watu wajipatie fedha. Alisema fedha hizo zilitokana na watumishi hewa Idara ya afya na elimu ambapo kulikuwa na watumishi wameacha kazi, kufa na wengine kuhama vituo vya kazi, lakini serikali iliendelea kulipa.
Aidha katika kipindi hicho mkoa huo ulipokea jumla ya malalamiko 248 kwa njia mbalimbali na kati ya hayo majalada 24 ya uchunguzi yanaendelea, yapo katika hatua mbalimbali. Frida alisema katika uongozi wa awamu ya tano umekuwa na ongezeko la wananchi kutoa taarifa nyingi tofauti na miaka ya nyuma, hali inayosababisha kupokea malalamiko yalio sahihi na yasio sahihi. Pia alisema katika kipindi hicho mashauri 14 yalisikilizwa na kati ya hayo 10 yalishinda katika kesi za jinsi na uhujumu uchumi

Dee Mzuri_Ft_Sun Rnb-Monalisa|daudimzuri

                             DOWNLOAD HAPA .